Karibu katika tovuti rasmi ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC). Tovuti hii itakusaidia kufahamu zaidi kuhusu Chuo chetu, huduma tunazotoa na mchango wetu katika kuimarisha utumishi wa umma nchini.

Katika TPSC, tunatoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wa umma na wadau wengine. Vilevile, tunafanya tafiti tumizi na kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu. Kupitia huduma hizi, tunalenga kujenga maarifa na stadi zitakazosaidia kuimarisha utumishi wa umma na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Ili kusogeza huduma karibu na wateja na wadau wetu, tuna kampasi sita zilizopo Dar es Salaam, Tabora, Mtwara, Singida, Tanga na Mbeya. Kupitia tovuti hii, utapata taarifa kuhusu programu za mafunzo, udahili, huduma na shughuli mbalimbali za TPSC.

Katika kutekeleza majukumu yetu, tunaongozwa na maadili ya kuthamini mteja, uadilifu, weledi, ubunifu, ushirikiano katika kazi na utoaji wa huduma bila upendeleo.

Ninakualika uvinjari tovuti yetu, upate taarifa unazohitaji na ufuatilie fursa mbalimbali zinazotolewa na Chuo.

Karibu TPSC. 

 

 

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo